BETI NASI UTAJIRIKE

JOHN BOCCO AZIDI KUWASHA MOTO SIMBA IKIIFUMUA MBEYA CITY


Klabu ya Simba SC imezidi kujisogeza jirani na taji la tatu mfululizo la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mshambuliaji John Raphael Bocco ameibuka nyota wa mchezo baada ya kufunga abao 2 yaliyoipa Simba alama tatu kwenye mchezo huo .Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 78, sasa ikiizidi pointi 20 Azam FC inayofuatia katika nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi 31.

Simba imebakiwa na pointi 3 tu sawa na mechi moja ili iweze kutangazwa bingwa mpya wa msimu wa 2019/20 . Endapo Simba itaibuka na ushindi dhidi ya Prisons basi itatangazwa bingwa mpya ikiwa jijini Mbeya na mchezo unaofuata itakwaana na Namungo mkoani mtwara.

Bocco alifunga bao la kwanza dakika ya tano akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama na la pili dakika ya 54 akimalizia pasi ya kiungo Mkenya, Francis Kahata Nyambura.

Post a Comment

0 Comments