advertise with us

ADVERTISE HERE

HUU SASA MSALA AKINA SAMATTA WAPIGWA TENA NA CHELSEA


Klabu ya Aston Villa kwa mara nyingine imepoteza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza kwa kuruhusu kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Chelsea. Mchezo huo uliopigwa dimba la Villa Park uliibua hisia kw mashabiki wa Soka hasa watanzania waliojiwekea matumaini ya Mbwana Samatta kufanya vizuri ndani ya Uingereza.

Aston Villa walikuwa wakwanza kupata bao la kuongoza kupitia Kortney Hause dakika ya 43 kipindi cha kwanza lakini chelsea walirudi kwa kasi zaidi kipindi cha pili na dakika ya 60 tu Pulisic akitokea sub alisawazisha bao hilo na dakika mbili baadaye Olivier Giroud aliandika bao la pili dakika ya 62.

Kwa matokeo hayo Chelsea inafikisha pointi 51 kwenye msimamo wa ligi ikicheza michezo 30 na kubaki nafasi ya nne huku Aston Villa ikibaki nafasi ya 19 na pointi 26. Mbwana Samatta alicheza mchezo huo lakini hakuonyesha uwezo mkubwa wa kuiokoa timu yake isishuke daraja.

Mechi nyingine ni ile ya New castle dhidi ya Shiffield United mchezo uliomalizika kwa Newcastle kushinda mabao 3-0 yaliyofungwa na Maximin dakika ya 55,Ritchie dakika ya 69 na Joelinton dakika ya 78. 

Matokeo hayo yanawafanya Newcastle wawe nafasi ya 13 wakiwa na pointi 38 wakicheza michezo 30 na Shiffield wanatelemka mpaka nafasi ya 7 wakiwa na pointi 44.

Post a Comment

0 Comments