advertise with us

ADVERTISE HERE

HIZI HAPA MECHI NNE KWA SIMBA KUTANGAZWA BINGWA
Klabu ya Simba inajiandaa vyema kuelekea kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo ligi kuu Tanzania Bara na wamebakiwa na mechi 10 huku wakitakiwa kushinda mechi 4 tu ili waweze kutangazwa kama mabingwa.

Hizi hapa ni mechi 4 za Simba kutangazwa ubingwa 

Simba vs Ruvu Shooting

Simba na Ruvu shooting watakutana tarehe 14 Juni dimba la Taifa na simba italaimika kushinda mchezo huo ili kujihakikishia inajiweka nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa.

Simba vs Mwadui FC

Mchezo huo utachezwa jijini Dar es salaam Simba wakiikaribisha Mwadui FC timu ya mkoani Shinyanga . Mchezo huo utapigwa tarehe 20 na  kama Simba atashinda mchezo huo litakuwa ni jambo la msingi kwa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Karikoo-Msimbazi.

Mbeya City vs Simba 

Mchezo huu utapigwa dimba la sokoine tarehe 24 Juni na kama simba akishinda basi atasubiri mechi na Prsons aweze kutangazwa bingwa mpya kwa msimu wa 2019/2020

Prisons vs Simba 

Endapo Simba atashinda michezo mitatu mfululizo basi akishinda mchezo huu atatangazwa kama bingwa mpya wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2019 /2020

kwa sasa Simba inaongoza ligi kuu Vodacom ikiwa na pointi 71 akifuatiwa na azam mwenye pointi 54 na Yanga 51 . Ushindi wa mechi 4 utaifanya kufikisha pointi 83 na hakuna timu inaweza kuzifikia 

Hii hapa ratiba kamili

Post a Comment

0 Comments