Wachezaji na makocha wa Ligi ya Primia ya England hawatalazika kuvaa barakoa uwanjani mara ligi hiyo itakaporejea wiki ijayo.
Hata hivyo wachezaji hawatatakiwa kutema mate uwanjani au kusafisha pua zao na kutokumbatiana wakati wa kushangilia magoli.
Pia hakutakuwa na watoto wa kuwarushia wachezaji mipira inayotoka nje, na badala yake mfumo maalumu wa mipira iliyosafishwa utatumika.
Aston Villa v Sheffield United utakuwa mchezo wa kwanza wa EPL utakaofungua tena pazia la EPL Juni 17.
Ligi hiyo ilisimamishwa mwezi Machi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Nchini Ujerumani wachezaji, makocha na Magila wengine wa ligi ya Bundesliga wanatakiwa kuvaa barakoa muda wote isipokuwa muda wa mechi.
Katika ligi ya EPL hawatatakiwa kuvaa barakoa kabisa, hata katika vyumba vya kubadili na kwenye mabenchi ya makocha na wachezaji wa akiba.
0 Comments