BETI NASI UTAJIRIKE

HAWA HAPA NYOTA SITA WA YANGA WATAKAOKOSEKANA LEO DHIDI YA AZAM


Yanga itakuwa na kibarua kizito mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa majira ya saa 10:00 Uwanja wa Taifa.Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa.

Itawakosa nyota wake nane kutokana na sababu mbalimbali namna hii:-Papy Tshishimbi nahodha wa Yanga bado hajawa fiti kwa sasa kucheza mechi za ushindani, Erick Kabamba, Ally Ally, Raphael Daud na Ramadhan Kabwili hawa hawapo kwenye mpango wa mwalimu.

 Ally Mtoni,'Sonso', na Said Juma Makapu hawa wawili wameshaanza kurejea kwenye ubora wao walikuwa wanaumwa ni kazi ya mwalimu kuamua kuwatumia ama la. 

Beki Lamine Moro anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa Juni 17 mbele ya JKT Tanzania wakati Yanga ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa Jamhuri.

Post a Comment

0 Comments