advertise with us

ADVERTISE HERE

HATIMAYE DAVID MOLINGA "FALCAO" AONDOKA DAR ES SALAAMMshambuliaji wa klabu ya Yanga David Molinga ameondoka leo asubuhi kuelekea mkoani shinyanga kuungana na wachezaji wenzake kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui.

Molinga  ameondoka na kocha mkuu wa timu hiyo Luc Eymael kuelekea jijini Mwanza kisha baadaye shinyanga.

Hapo awali mshambuliaji huyo aligoma kusafiri na timu kwa kile kinachodaiwa jina lake halikutajwa kwa wachezaji watakosafiri na timu hiyo suala lililoibua mvutano mkali kati ya Uongozi na mchezaji huyo.Mkataba wa Yanga na Molinga unamalizika mwisho wa msimu na pande zote hazijaridhia kuurefusha.

Mchezo wa Yanga na mwadui utapigwa hapo kesho saa 10 jioni na utarushwa live kupitia azam TV.Post a Comment

0 Comments