BETI NASI UTAJIRIKE

FAROUK SHIKHALO AKUBALI UWEZO WA METACHA MNATA


Golikipa namba mbili wa kikosi cha Yanga Farouk Shikhalo amefunguka ishu ya kuwekwa bechi na kipa Metacha Mnata. Kipa huyo aliyesajiliwa kutoka Bandari kenya amekuwa na wakati mgumu kuanza kwenye mechi mbalimbali kutokana na kiwango kizuri kinachoonyeshwa na kipa namba moja wa sasa Mnata.

Itakumbukwa msimu wa 2018/19 kipa huyo aliitwaa tuzo ya kipa bora ligi kuu nchini Keny lakini kwa hapa tanzania amekuwa akipigwa benchi na Metacha mnata. Kipa huyo amefunguka kwa kusema 

Kila mchezo una falsafa zake na mwalimu anajua ni nani anastahili kuanza kwenye mechi husika, kukaa kwangu benchi haina maana kwamba siwezi hapana ni maamuzi ya mwalimu na kwa hali hiyo inanifanya nizidi kupambana ili kuwa bora,” alisema Shikhalo

Post a Comment

0 Comments