EYMAEL AFICHUA KINACHOIKWAMISHA USHINDI YANGA


Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema kuwa tatizo kubwa walilonalo wachezaji wake wote kwa sasa ndani ya kikosi ni kushindwa kumalizia nafasi ambazo wanazitengeneza ndani ya uwanja.

Juni 24, Yanga ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa jambo ambalo lilimkasirisha raia huyo wa Ubelgiji.

Mabao ya Yanga yalifungwa na David Molinga ambaye ni mtupiaji namba moja ndani ya klabu hiyo akiwa na mabao 10 kibindoni huku yale ya Namungo yakipachikwa kimiani na Edward Manyama.

Sare hiyo inawafanya Yanga wasalie nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 57 huku Namungo ikibaki nafasi ya nne baada ya kufikisha pointi 56 na zote zimecheza mechi 31.

Eymael amesema:"Haikupaswa tupate sare mbele ya Namungo tena kwa shida kubwa hii ni hatari kwetu na haipendezi, unajua tulipaswa kumaliza mchezo kipindi cha kwanza tulipata nafasi tatu za wazi ambazo tungefunga kazi ilikuwa imeisha.

"Ninashangazwa na wachezaji wangu wanafika karibu na eneo la hatari wanapata nafasi wakiwa na mpira wanakopiga wanajua wenyewe sasa mimi nitafanyaje katika hilo?

"Haipo hapa Tanzania tu hata Ulaya pia mambo haya yanatokea lakini naona hili tatizo linazidi kuwa kubwa, nina uwezo mkubwa wa kufundisha lakini ninakwamishwa na wachezaji wangu katika maamuzi yao ndani ya uwanja," amesema.

Mchezo uliopita mzunguko wa kwanza walipokutana na Namungo Uwanja wa Majaliwa, Yanga ilianza kushinda bao 1 kupitia kwa Tariq Seif likapinduliwa na Bigirimana Blaise.

Mzunguko wa pili, Namungo walianza kupitia kwa Manyama, Molinga akamaliza kwa Yanga na kufanya wagawane pointi mbili na kuziyeyusha pointi nne katika sita kwa kila timu.

Post a Comment

0 Comments