CHELSEA FC VS MANCHESTER CITY UPO UPANDE GANIKlabu za Chelsea na Manchester City zinajitupa dimbani hii leo kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza.  Chelsea ikiwa nyumbani kwa mchezo wake wa 31 ikiwa na pointi 51 nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu italazimika kushinda mchezo huo ili iweze kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa ulaya msimu wa 2020/21.  klabu ya Manchester City itatua jijini London kusaka pointi kwenye mchezo wake wa 31 ikiwa na matumaini ya kuchukua pointi hizo ili kuendelea kufukuza ubingwa wa ligi kuu Uingereza kwa msimu huu.

Mchezo huo wa kukata na shoka utapigwa saa 10:15 usiku katika dimba la Stamford Bridge na mashabiki wa soka duniai kote watakuwa wkiusuhusia kupitia Runinga zao. 

Mara ya Mwisho kwa Chelsea kuifunga Manchester City ni mwaka 2018 walipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 huku wakiwa na kumbukumbu ya kupigwa mabao 6-0 mwaka 2019 .

Post a Comment

0 Comments