Uongozi wa Yanga umesikitishwa na tabia za ajabu zilizoanzishwa na mashabiki wa klabu hiyo hivi karibuni. Hapo jana mara baada ya mchezo kati ya Yanga na Azam mashabiki walilivamia basi la wachezaji wakitaka uongozi umuondoe kikosini mshambuliaji wao Yikpe. Suala hilo halikuishia hapo tu kwani mmoja wa mashabiki wa klabu hiyo anayejulikana kwa jina la Mzee wa Utopolo alipigwa na baadhi ya mashabiki wliodai anaichafua klabu kwa kauli zake .
Leo uongozi wa klabu hiyo umetoa tamko kulaani kitendo cha mashabiki hao pia kwa vyombo vya habari vinavyotoa taarifa za kichochezi zenye lengo la kuharibu amani ndani ya klabu, ugomvi kati ya wachezaji na mashabiki, Ugomvi kati ya mashabiki
0 Comments