BAYERN MUNICH YATWAA TENA UBINGWA BUNDESLIGAMabingwa watetezi wa Bundesliga Bayern Munich wametwaa tena ubinwa wa ligi hiyo kwa mara ya nane mfululizo. Bayern Munich wametaa ubingwa huo wakiwa na pointi 76 baada ya kucheza michezo 32 na wakibakiwa na michezo mingine miwili ya kumalizia ligi

Bao la Robert Lewandowski dakika ya 43 dhidi ya Werder Bremen lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.Kadi nyekundu aliyopewa Alphons Davies haikuwa kikwazo kwa Bayern Munich kushinda mchezo huo uliomalizika kwa Bayern Munich kushinda 1-0. 

Bayern Munich imetwaa ubingwa wa 8 mfululizo bila kuumzika kutoka mwaka 2012 mpaka 2020 na kuifanya kutimiza makombe 29 ya Bundesliga huku ikiendelea kuweka rekodi ya kuogoza kwa wingi wa makombe hayo kuliko klabu yeyote. 

Robert Lewandowski anabakia kinara wa Ufungaji akiwa na mabao 31 akifuatiwa na Timo Warner mwenye mabao 25 

Post a Comment

0 Comments