Simba walilazimshwa sare ya mabao 1-1 na matokeo hayo yamewafanya kuendelea kuongoza ligi kuu baada ya kufikisha alama 72
Leo asubuhi kikosi hicho kimecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp dimba la uhuru jijini Dar es salaam na mchezo huo umemalizika kwa Simba kushinda mabao 4-0.
Ibrahim Ajibu alikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za transit camp dakika ya 16 huku Gerson Fraga akifunga mabao mawili dakika ya 31 na 45 na Cyprian Kipenye akifunga bao la nne dakika ya 86.
Simba inajiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui mchezo utakaopigwa siku ya jumamosi tarehe 20 wiki hii
Picha za mechi kati ya Simba vs Transit Camp
0 Comments