AZAM FC WALIBANA KWA YANGA WAMEACHIA KWA KAGERA


Klabu ya Azam FC imekumbana na kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera sugar kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa dimba la Kaitaba mkoani Kagera. Mchezo huo unaifanya Azam kubaki na pointi 58 nyuma ya Simba wenye pointi 78 huku wakiizidi Yanga pointi 1 wakiwa nafasi ya tatu na pointi 57.

Bao la Yusuph mhilu liliisaidia Kagera Sugar kufikisha pointi 44 kwenye michezo 31 huku wakiwa nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara. 

Azam wamejikuta wakishindwa kuongeza pointi 3 muhimu baada ya kucheza mechi 2 wakiambulia pointi 1 na ikumbukwe mchezo dhidi ya Yanga walicheza kwa kiwango kikubwa na kutoka sare ya 0-0  lakini wameshindwa kuhimili mikiki ya Kagera Sugar.

Kagera wamekuwa wakali hasa wanapokutana na timu kama Simba,Yanga na Azam na hilo lilidhihirika baada ya kuifunga Yanga mabao 3-0 kwenye mzunguko wa kwa wa ligi kuu Tanzania Bara huku wakijiandaa kukutana tena kwenye mchezo wa FA .


Post a Comment

0 Comments