advertise with us

ADVERTISE HERE

ARSENAL KAMA KAWAIDA WAMEPIGWA TENA


Klabu ya Arsenal imepokea kipigo cha nane msimu huu baada ya kufungwa mabao 2-1 na Brighton ligi kuu nchini Uingereza. Hii inakuwa  wiki chungu kwa kocha wa timu hiyo Mikel Arteta baada ya kupokea kipigo cha 3-0 kutoka kwa manchester City

Arsenal walikuwa kupata bao la kuongoza dakika ya 68 kupitia mshambuliaji Nicolas Pepe lakini bao hilo halikudumu kwani mshambuliaji wa Brighton Lewis Dunk alisawazisha bao hilo dakika ya 75 na dakika za lala salama Neal Maupay alishindilia goli la ushindi dakika ya 90 ya mchezo 

Matokeo hayo yanaifanya Arsenal ushuka mpaka nafasi ya 10 wakiwa na pointi 40 huku wakibakiwa na michezo 8 kuweza kufuzu nafasi ya nne . swali ni je wataweza?

Post a Comment

0 Comments