Arsenal inatarajiwa kuanza mazungumzo na wakala wa kiungo wa kati wa Barcelona Phillipe Coutinho.
Mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 amehudumia msimu wote akiwa kwa mkopo katika mabingwa hao wa Ujerumani Bayern Munich, lakini klabu hiyo haiko tayari kulipa paundi milioni 105 za Uingereza ili kufanikisha mkataba wa kudumu.(Le10sport - in French)
Paris St-Germain inafanya mazungumzo na Arsenal katika jaribio la kumsaini mashambuliaji wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang, 30, for £34m. (Todofichajes)
Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 32, huenda akarudi katika ligi ya premia baada ya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Chelsea - Newcastle na Wolves zote zinamwania. (Express)
Mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 24, amehusishwa pakubwa na uhamisho wa kujiunga na Liverpool lakini aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United Owen Hargreaves anahisi kwamba uhamisho wa klabu hiyo ya Old Trafford ungekuwa bora zaidi kwa mchezaji huyo. (Star)
Mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez, 29 mwenye thamani ya £57m, ananyatiwa na Manchester United, Arsenal na Real Madrid. (Tuttosport - in Italian)
Mshambuliaji wa Bournemouth Joshua King, 28, analengwa na klabu sita zilizopo katika uongozi wa ligi ya Premia baada ya ombi la dau la paundi millioni 20 katika siku ya mwisho ya uhamisho kukataliwa mnamo mwezi Januari. (Mirror)
Juventus inataka kuipiku Real Madrid katika ununuzi wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 19, katika uhamisho wa dau la £67m. (Tuttosport - in Italian)
Barcelona iko tayari kumuuza mashambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kwa dau la £37m. Klabu hiyo ya Uhispania ililipa £137m kumnunua raia huyo wa Ufaransa miaka mitatu iliopita lakini ameanzishwa mara tano pekee kufuatia msururu wa majeraha. (Mirror)
Winga Adama Traore, 24, ameshauriwa kuipuuza hamu ya Liverpool na kusalia katika klabu ya Wolves kwa msimu mwengine na mchezaji wa zamani wa Sheffield United Michael Brown. (Star)
Winga wa Wales na klabu ya FC Schalke Rabbi Matondo, 19, anasema kwamba amejiandaa vilivyo kujiunga na klabu hiyo ya Ujerumani huku kukiwa na hamu kutoka kwa Manchester United. (Manchester Evening News)
0 Comments