TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 18-5-2020

Juventus inakaribia kuafikia makubaliano ya kumsaini Paul Pogba,27 kutoka klabu ya Manchester United na itajaribu kumtumia kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 25, ili kupunguza bei hiyo. (L'Equipe, via Sunday Express)
Lakini mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane bado ana matumaini ya kumsaini mchezaji huyo kutoka Manchester United. (Mundo Deportivo, via Star on Sunday)
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe hatalazimisha kuondoka katika klabu ya PSG mwisho wa msimu huu kutokana na madhara ya kifedha ya mlipuko wa corona, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atasalia na mabingwa hao wa ligue 1 kwa msimu mmoja zaidi.(L'Equipe, via AS)
Barcelona na Real Madrid zinamnyatia winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho lakini Manchester United wamekuwa katika mstari wa mbele kujaribu kumsaini mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 20. (Athletic, via Star on Sunday)
Wakati huohuo Chelsea inatarajiwa kupokea £48.5m kutoka kwa Atletico Madrid kwa mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata 27 mwisho wa msimu huu na inaweza kutumia fedha hizo kumuandama Jadon Sancho . (Sun on Sunday)
MbappeHaki miliki ya pichan
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amesifu mchezo wa mshambuliaji wa Inter Milan na mchezaji mwenza wa Argentina Lautaro Martinez, 22, ambaye ametajwa kama mchezaji anayelengwa na klabu hiyo ya Uhispania. (Sport, via Metro)
Mkufunzi wa Club Bruges Philippe Clement amesema kwamba anataraji kwamba mshambuliaji wa Nigeria mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Nigeria Emmanuel Dennis, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Arsenal, Newcastle United na Wolves, ataondoka katika klabu hiyo. (La Derniere Heure, via Birmingham Mail)
Wakati huohuo aliyekuwa kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Xavi hadhani kwamba mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane 28, na mshambuliaji wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang anayechezea Arsenal wanaweza kuingiana na soka inayochezwa katika uwanja wa Nou Camp . (Metro)
Sadio ManeHaki miliki ya picha
Beki mkongwe wa Juventus na Italy Giorgio Chiellini amesema kwamba uamuzi uliofanywa na beki wa kati wa Real Madrid Sergio Ramos kumkabili visivyo mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah ambao ulimlazimu nyota huyo kutolewa uwanjani kutokana na jeraha katika mechi ya fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya 2018 ulikuwa uamuzi wa 'kijanja'. (Marca)
Chelsea inaamini iko katika mstari wa mbele zaidi ya Tottenham katika harakati zao za kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 16 Lamare Bogarde, anayechezea klabu ya feyenood

Post a Comment

0 Comments