RAGE AZUNGUMZIA KUKAMATWA KWAKEMwenyekiti wa zamani Simba bwana Ismail Rage amesema kuwa hajaamua mpaka sasa kama atagombea ubunge ama hatagombea kwa kuwa anapima upepo ajue mambo yatakuaje.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni baada ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa kudaiwa kuwa alikuwa ameanza kufanya kampeni za siri jambo ambalo ni kinyume na katiba.

Rage ambaye ni mbunge wa zamani wa Tabora Mjini, aliwekwa mahabusu kuanzia Mei 23 hadi Mei 24 ambapo aliachiwa kwa dhamana.

Rage amesema:-"Nikawauliza iweje tangu tangu tarehe 16 mje kunihoji leo siku 73 zimepita? Kwanza mimi sijatangaza nia mpaka sasa wala sijaamua kwamba nitagombea au sitagombea. Napima upepo kwanza. Mimi kwetu Tabora na bahati mbaya mbunge ambaye yupo sasa hatokei Tabora sasa nahisi labda ana hofu na mimi."

Post a Comment

0 Comments