BETI NASI UTAJIRIKE

MBAPPE VS BEN YEDDER NANI ANASTAHILI KUWA MCHEZAJI BORA LIGUE 1 KWA MSIMU WA 2019/2020?




Ligi kuu Ufaransa ilimalizika mapema baada ya janga la Covid 19 kushika kasi barani Ulaya . Chama cha soka Ufaransa (France Football Federation ) kilifikia muafaka kwa kumaliza msimu kukiwa kumebakiwa na mechi 10 kwa kila timu na ubingwa walikabidhiwa PSG . 

Maswali yaliibuka ni nani atatwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligue 1 kwa msimu wa 2019/20. Wengi wanaamini Mbappe anastahili kutwaa tuzo hizo lakini binafsi siafiki mchezaji huyo kutwaa tuzo . Hizi ni takwimu za Mbappe kwa msimu huu.

Ufungaji wa mabao 

Kylian Mbappe na Ben Yedder wote kwa pamoja wamefunga mabao 18 wakifuatiwa na Dembele aliyefunga mabao 16 kisha Neymar mabao 13 na Osmhen mabao 13

Utengenezaji mabao 

Di maria anaongoza orodha ya watengeneza mabao akitengeneza nafasi 14 huku akifuatiwa na Slimani nafasi 8,Lees na neymar wamefungana kwa nafasi 6 huku Mbappe,Ben Yedder,Simon,na Laborde wakitengeneza nafasi 5 

Swali ni je nani anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora ?

Dimaria amehusika kwenye mabao 22 ya PSG , Ben Yedder amehusika mabao 23 ya Monaco sawa na Mbappe 23 kwa PSG

Kama kitatumika kigezo cha timu kutwaa Ubingwa basi Mbappe atapewa tuzo hiyo lakini kikitumika kigezo mchezaji binafsi  basi wachezaji Mbappe na Yedder wanastahili tuzo 

Post a Comment

0 Comments