ads

adds

MAKALA: HALAAND VS LEWANDOWSKI NANI KUONEKANA BORA LEO

Bayern Munich inakaribishwa na Borrusia Dortmund  dimba la Signal Idua Park hii leo majira ya saa 7:30 .Mashabiki wa soka duniani kote wamehamia Ujerumani kufahamu nini kitatokea  siku hii ya leo. Nimekuwekea uchambuzi kwa timu hizo


1. Vita ya Borrusia Dortmund vs Bayern Munich 

Timu hizo zimekutana mar 103 huku Bayern Munich akishinda mara 48 sare 29 na kufungwa michezo 26 tu. Takwimu hizo zinaifanya Dortmund ionekane "underdog" kwa Bayern munich 

Michezo  mitano iliyopita kat ya timu hizo Bayern Munich amefkuwa kinara kwa kushinda michezo 3 kati ya 5 huku akitoa kipigo cha mabao 6-0 

2. Msimu wa 2019/2020

Bayern Munich hajapoteteza mchezo wowote tangu kuanza kwa mwaka 2020  na kumfanya akae kileleni kwa pointi 61 kati ya 57 za Dortmund.

Timu hizo zimecheza mechi 27 kila mmoja na Bayern Munich ameshinda 19 sare 4 na kufungwa 4 huku wakifunga mabao 80 na kufungwa mabao 28 

Borrusia Dortmund ameshinda michezo 17 akipata sare 6 na kufungwa 4 huku aifunga mabao 74 akifungwa mabao 33 

Bayern Munich anaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 4 na kama atashind mchezo huu basi atajihakikishia kutwaa ubingwa wa Bundesliga.

3. Kombinesheni ya ushambuliaji

Bayern Munich wanaongozwa na Robert Lewandoski  mwenye mabao 27 huku Borrusia Dortmund wakimtegemea Sancho mwenye mabao 14 tu . Thomas Muller anaongoxa kwa kutoa usaidiza wa mabao akifanya hivyo mara 17 huku sancho akifanya hivyo mara 16. Watu wanaotazamiwa kwenye mchezo huu ni pamoja na Haaland na Gnabry 

4.Mechi baada ya Lockdown 

Bundesliga ni ligi ya kwanza kurejea mara baada ya locdwn kwa mataifa ya ulaya . na mpaka sasa wamecheza mizunguko miwili. Dortmund vs schalke o4 waliibuka na ushidi wa mabao (4-0) na mchezo wa pili Borrusia walishida 2-0 dhidi ya Wolfsburg. 

Bayern Munich amecheza dhidi ya Union Berlin na kushinda 2-0 huku mchezo wa pili aakishinda 5-2 dhidi ya Frankfurt 

Mchezo wa leo ni raundi ya 3 je nani ataibuka mbabe 

5. Halaand vs Lewandowski

Ni ngumu sana kumfananisha Lewandowski na mshabuliaji kama Halaand kutokana na ubora alionao lakini uwezo wa kitakwimu wachezaji hawa wanaonekana kufanya vizuri kwa pamoja . Halaand amecheza michezo 13 akiwa na Borrusia Dortmund na alifanikiwa kufuna mabao 13 . Lewandowski akiwa na Bayern Munich amecheza michezo 27 akifunga mabao 27 kwa ratio hiyo washambuliaji wot wanaonekana kufunga kila mechi wanayocheza.

Post a Comment

0 Comments