Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema wachezaji ambao hawafanyi mazoezi kama wanavyoelekezwa, ligi itakaporejea watajulikana.Matola ameeleza kuwa wapo wachezaji ambao wanazembea program ambazo wamepewa na benchi la ufundi, jambo lisilopendeza
Matola alisema ligi ikirejea wachezaji wazembe watakuja kuumbuka, kwani watashindwa kuonesha walichokuwa wanafanya wakiwa nyumbani."
"Mchezaji anayejitambua na anayependa kazi yake hawezi kukubali awe anasimamiwa kila wakati ila kwa wale ambao bado wanapuuzia muda wao unakuja kwani ligi ikirejea watajulikana tu kwa matendo wataumbuka,” alisema Matola
Matola amewataka wachezaji wazingatie mazoezi waliyopewa kwa kuwa wana kazi kubwa ya kutetea ubingwa wao.
Hivi karibuni benchi la ufundi la Simba likiongozwa na kocha Sven Vandenbroeck lilikutana na wachezaji wa timu hiyo ambapo pamoja na mambo mengine waliweka mkakati wa kjiweka tayari kwa kurejea kumalizia mechi zilizobaki pale Serikali itakapotoa ruhusa
0 Comments