YANGA inaelezwa kuwa ipo kwenye hesabu za kuboresha kikosi chake msimu ujao ambapo kuna nyota zaidi ya 10 wamewekwa kwenye rada kutua hapo msimu ujao. Nyota wanaotajwa kuwekwa kwenye rada za Jangwani ni pamoja na:-Straika wa Namungo FC, Reliants Lusajo na Bigirimana Blaise, beki wa kati wa Coastal Union ya Tanga, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Ame, kiungo wa kati wa Polisi Tanzania, Baraka Majogoro, mlinzi wa kushoto, Yassin Mohamed na Sixtus Sabilo mshambuliaji. Hawa hapa ni wa kimataifa winga wa AS Vita ya DR Congo, Tuisila Kisinda, kiungo mkabaji Ally Niyonzima raia wa Rwanda, anayekipiga Rayon Sports ya nchini humo, pia kuna Heritier Makambo anayekipiga Horoya AC ya nchini Guinea. Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hesabu za msimu ujao ni kubwa wanaimani watasuka kikosi cha ushindani ila ni mpaka pale usajili utakapofunguliwa.
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments