BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA YAJIANDAA KUHAMIA KIGAMBONI



Wakati mchakato wa ujenzi wa Complex ya Yanga huko Kigamboni ukiendelea,uongozi wa timu hiyo utaanza na kukamilisha uwanja wa mazoezi ili kupunguza gharama za kukodi viwanja, imefahamika

Imeelezwa kampuni ya GSM ambayo ndiyo inayogharamia viwanja na Hostel, itasimamia kukamilishwa kwa uwanja huo ili kuanzia msimu ujao utumike
Kampuni hiyo inatumia hadi Tsh laki tano kwa siku kulipia gharama za viwanja ambavyo Yanga huvitumia

Awali Yanga ilipanga kukamilisha uwanja wake pale Jangwani ambapo zoezi la kumwaga kifusi lilikuwa liko hatua za mwisho

Hata hivyo Serikali iliutaka uongozi wa Yanga usitishe mradi huo kwa kuwa Serikali imeweka mkakati wa kudhibiti mafuriko eneo la Jangwani.Mradi huo utaendelea baada ya Serikali kudhibiti changamoto ya mafuriko Jangwani

"Ni kweli upo mpango wa kutengeneza uwanja wa mazoezi kule Kigamboni. Tulikuwa na zoezi hilo hapa Jangwani lakini Serikali ilituagiza tusitishe kwa kuwa kuna mradi mkubwa wa kudhibiti mafuriko," alisema Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela

"Uzuri kule Kigamboni tunalo eneo zuri ambalo halitachukua gharama kubwa kulikarabati. Tutatengeneza uwanja wa mazoezi wakati mchakato wa mradi mkubwa ukiendelea"

Post a Comment

0 Comments