BETI NASI UTAJIRIKE

WAZAZI TUZINGATIE HUU SI WAKATI WA KUMTAFUTA MBWANA SAMMATA MPYA

Tunazidi kuwa kwenye wakati mgumu kwa sasa kutokana na kila mmoja  kuwa na hofu ya kusambaa kwa Virusi vya Corona kitu ambacho kitaalamu kinapoteza uwezo wa asili wa kupambana  kutafuta suluhisho.

Kwa sasa bado janga kubwa la dunia ni kusambaa kwa Virusi vya Corona ambapo mgonjwa wa kwanza  kugundulika alitokea nchini China ilikuwa Desemba,2019.

Kila mmoja amekuwa akiripoti namna anavyotambua kuhusu Corona ila kinachotakiwa ni kuacha kuwa na hofu na kuamini kwamba ugonjwa upo lazima tuchukue tahadhari.

Nyakati ngumu pia huwa inakuwa vigumu kupata majibu sahihi iwapo kila mmoja atataharuki kutafuta majibu anayoyataka ni lazima tutulie na kuendelea kuomba ili mambo yapite salama.

Kwa wachezaji ambao kazi yao kubwa ni kucheza kwa sasa wapo kwenye mapumziko ya lazima kwani Ligi Kuu Bara nayo imesimamishwa na Serikali ili kuzuia maambukizi zaidi.

Kwa upande wa wanafunzi tunaona kwamba shule zimefungwa ikiwa ni pamoja na vyuo lengo ni moja kuzuia maambukizi zaidi kwani afya ni utajiri wa kwanza.

Mambo yamekuwa tofauti kwa baadhi ya wazazi na walezi wameacha suala hili mikononi mwa Serikali bila kujali afya za watoto.

Baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaacha watoto kwenye mijumuiko isiyo ya lazima na wanafunzi hao wanaendelea kucheza mpira ama kuwa kwenye mikusanyiko ya watu wengi jambo ambalo linapaswa lichukuliwe tahadhari.

Katika hili kila mmoja jukumu ni lake kuhakikisha anakuwa balozi mzuri kwa kulinda afya ya mtoto pamoja na jamii nzima kiujumla kwa ajili ya tahadhari ya Virusi vya Corona.
Tusisubiri kila sehemu tukumbushwe na Serikali, gharama za matibabu ni kubwa muhimu kwa sasa kuchukua tahadhari.
Wale ambao wamekuwa wakijali na kuwapa elimu wanafunzi nawapongeza kwani sio wote hawajali hapana wapo ambao wanajali lakini wachache wanaoacha hili lazima lidhibitiwe.
Kuwaruhusu waendelee kucheza ni hatari iwapo itatokea maambukizi basi kasi ya kusambaa itakuwa kubwa na gharama zake pia zitaongezeka.
Wachezaji pia muda wa kuendelea kufanya mazoezi ya kujiimarisha ili kulinda kipaji ni muhimu kwa kufuata program ambazo mmepewa na walimu wenu.
Pia kwa wale ambao hawajapewa bado wanaweza kujipa mazoezi wenyewe wakiwa nyumbani kwani bado wana muda wa kufanya mazoezi kabla ya ligi kurudi.
Iwapo mchezaji atashidwa kujipa mazoezi yeye mwenyewe wakati ligi itakapoanza atashindwa kuendelea pale alipoishia itamchukua muda mrefu kurudi kwenye ubora.
Kinachotakiwa ni kuchukua tahadhari na kufanya mazoezi pamoja na kuzingatia maelekezo ambayo mmepewa na makocha.
Kila mmoja akichukua tahadhari itasaidia kupunguza maumivu pale maambukizi yatakapotokea na kila mmoja atakuwa katika usalama.
Elimu inabidi iendelee kutolewa kuhusu janga hili ili kila mmoja atambue vizuri kwani inaonekana kuna baadhi ya maeneo hasa ya kule vijijini bado hawajapata taarifa sahihi.
Wakati huu kwa wale ambao watakuwa wanatoka mjini na kuelekea vijijini wawe mabalozi wazuri katika hili na wafanye jitihada kuwapa taarifa sahihi kwa kile abacho wanauhakika nacho ikiwa ni ngumu basi wazungumze na wataalamu wa afya.
Kwa wale wataalamu wa afya wasichoke kuzungumza na watu wao na kuwapa tahadhari pia kwani wengi bado wanadhani ni kitu cha kawaida jambo ambalo linawafaya wasichukue tahadhari.
Mungu atufanyie wepesi katika hili suala ambalo lilianza kama utani lakini kwa sasa limekuwa ni janga.
Wachezaji bado nitazidi kuwaambia kwamba wasisahau kufuata maelekezo ambayo wamepewa na makocha wao kwa kuendelea kulinda vipaji vyao kwa kufanya mazoezi.
Afya yao pia ni suala la kuzingatia kwa kuchukua tahadhari jambo litakalowafanya wawe salama katika wakati huu ambao nina amini ni wa mpito.
Ni wakati ambao kila mmoja anatakiwa kuwa makini na kufuata tahadhari ya kile ambacho anaambiwa ili awe salama.

Post a Comment

0 Comments