Pamoja kufanya nae mazungumzo ya pili ili kumuongezea mkataba, uongozi wa Yanga umekiri bado nahodha wake Papi Tshishimbi hajarejesha mkataba huo.Hivi karibuni Tshishimbi alifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Yanga Dk David Luhago ambapo baadae alionana na mabosi wa GSM
Inaelezwa Tshishimbi alipewa ofa nono zaidi ya ile ya kwanza ikiambatana na mkataba wa miaka miwili.Katika mapendekezo yake ya kwanza inaelezwa Tshishimbi alitaka dau la usajili linalofikia Tsh Milioni 150 na mshahara wa Tsh Milioni 18 mapendekezo ambayo hayakuridhiwa na uongozi wa Yanga wala wadhamini wao GSM
Lakini baada ya mazungumzo ya pili Tshishimbi aliridhia ofa aliyopewa na kuahidi kusaini mkataba huo
Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema bado Tshishimbi hajarejesha mkataba huo
"Tshishimbi tulishamalizana nae, ameshakabidhiwa mkataba ulionona, bado hajaurejesha akiwa ameusaini. Tunaamini atamwaga wino muda si mrefu," alisema
Mashabiki wa Yanga wameonyesha wasiwasi kutokana na 'danadana' hizo zinazofanywa na Tshishimbi
Msimu uliopita Gadiel Michael alikabidhiwa mkataba, akakaa nao mpata siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa ikabainika kuwa alikuwa amesaini klabu ya Simba
Ni baada ya Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla kumpa masaa 24 awe ameurejesha mkataba huo akiwa ameusaini
Mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga ameutaka uongozi wa timu hiyo wamuwekee Tshishimbi muda mapema awe amerudisha mkataba huo ili akishindwa kufanya hivyo waachane nae
"Hatujasahau alichotufanyia Gadiel. Timu yetu msimu huu haiko vizuri upande wa kushoto ni kwa sababu yake. Viongozi walimuamini na kumuachia mkataba akae nao siku zote hizo lakini mwishoni wakati dirisha la usajili linakaribia kufungwa akasaini Simba... Wakati huo Yanga haikuwa na muda wa kutosha kusaka mbadala wake"
"Apewe hata wiki moja tu inatosha akishindwa kusaini basi tuachane nae, tutakuwa na muda wa kutosha kusaka mbadala wake.."
0 Comments