Barcelona wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kutoka klabu ya Inter Milan lakini wanakabiliana na ushindani mkali kutoka kwa Real Madrid na Manchester City. (Marca)
Klabu ya Wolves haitamuuza Adama Troare, 24, kwa dau lolote chini ya pauni milioni 70 huku winga huyo akihusishwa na mipango ya kuhamia Liverpool. (Football Insider)
Arsenal wanalenga kumsajili beki wa Athletic Bilbao Unai Nunez, 23, kama kipaumbele chao kwa usajili wa majira ya kiangazi. Beki huyo wa Uhispania ana kifungu cha mkataba kinachoelekeza kuuzwa kwa euro milioni 30. (La Razon - in Spanish)
Shirikisho la mpira duniani Fifa linapanga kuongeza muda wa moja kwa moja wa msimu wa 2019-20 ili kuruhusu kila nchi kuamua ni lini msimu huo utaisha. (The Athletic - subscription required)
Liverpool, Manchester City na Manchester United wote wameonesha nia ya kumsajili winga wa Uhispania na Valencia Ferran Torres, 20. (Goal)
Kiungo wa Manchester United Jesse Lingard, 27, hana mpango wa kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu. Kiungo huyo anahusishwa na uhamisho kuelekea Arsenal na Everton. (Metro)
Liverpool wanakusudia kutuma ofa mbili za usajili kwa kiungo wa Uswizi Denis Zakaria na mshambuliaji wa Ufaransa Marcus Thuram wote kutoka klabu ya Borussia Monchengladbach. (Express)
Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, amefanya mazungumzo ya awali juu ya kuongeza mkataba katika klabu ya Chelsea. (Football.London)
Chelsea pia inajipanga kushindana na Arsenal katika mbio za kumsajili beki yaw a Ujerumani Jerome Boateng, ambaye anakaribia kuingia katika miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na klabu ya Bayern Munich. (Mail)
0 Comments