Kocha Msaidizi wa Simba Seleman Matola amesema kuwa wachezaji wa Simba kabla ya kuvunja kambi walifanyiwa vipimo vya uzito hivyo atakayeongezeka kilo ghafla hatua itachukuliwa. Hatua hiyo imefikiwa kutokana na kambi za timu kuvunjwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali ilizuia mikusanyiko isiyo ya lazima. Matola amesema:"Tunatambua kwamba kwa mazingira ambayo tupo itakuwa ngumu kuwadhibiti wachezaji kwa upande wa vyakula ila tuliwapima uzito hilo lipo kwenye rekodi. "Mchezaji ambaye ataonekana ameongezeka kilo ghafla itakuwa ni rahisi kutambua kwamba hakufuata program aliyopewa hivyo hatua juu yake itachukuliwa," .
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments