MORRISON ASIMULIA ALIVYOMFUNGA AISHI MANULA


kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa hakutarajia kumfunga mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula kwenye mchezo wa dabi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Machi 8.
Kwenye mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 na mfungaji alikuwa ni Morrison alifunga bao hilo dakika ya 44 baada ya kuchezewa rafu na Jonas Mkude nje kidogo ya 18.
Ushindi huo uliifanya Yanga isepe na pointi nne mazima mbele ya Simba msimu huu wa 2019/20 na mabao matatu kwani kwenye mchezo wa kwanza Januari 4 Uwanja wa Taifa waligawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 2-2 na mchezo wa pili Yanga ilishinda.
Morrison amesema:”Unajua mimi sina utaalamu wa kupiga mipira iliyokufa hivyo niliamua kupiga bila kufikiria nini kitatokea kwani ninamtambua mlinda mlango kazi yake kuzuia hivyo sikudhani kama ningefunga.
Bahati nzuri niliukuta mpira nyavuni hilo lilinishangaza na kunifurahisha, furaha ilikuwa kubwa kwa mashabiki na wachezaji hata tulipoingia ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo furaha ilikuwa kubwa,” alisema.
Morrison akiwa amecheza mechi 10 za Ligi Kuu Bara sawa na dakika 900 amehusika kwenye jumla ya mabao sita ya Yanga kati ya 31 akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.

Post a Comment

0 Comments