advertise with us

ADVERTISE HERE

MFAHAMU MCHEZAJI MSOMI ZAIDI WA MBAO FC
Mshambuliaji wa Mbao FC Wazir Junior ni mmoja ya washambuliaji hatari kwa msimu huu wa 2019/20 na hilo lilithibitik baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mwezi Novemba 2019 alipoifungia Mbao FC mabao 4 kwenye michezo mi4 ya mwezi Novemba.


Mbali na timu yake kushika nafasi ya 19 ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza michezo 28 lakini wazir JR amehusika kwenye mabao 9 kati ya yaliyofungwa na timu hiyo.

Wazir anatajwa kama ni mmoja ya wachezaji wachache wenye elimu kubwa akiwa na Digrii ya Technolojia na Mawasiliano (IT). Mshambuliaji huyo aliwahi kuichezea klabu ya Azam FC  kwa msimu wa 2017-2019 lakini hakudumu kwenye klabu hiyo yenye makao makuu Chamanzi na sababu kubwa ni majeraha ya mara kwa mara.

Kabla ya kutua Azam FC kisha Mbao mshambuliaji huyo aliania soka lake katika klabu ya Toto Afrika ya jijini mwanza 

Post a Comment

0 Comments