MFAHAMU IDD SELEMANI MAARUFU KAMA RONALDO WA BONGOAnaitwa Idd Seleman, mashabiki wameenda mbali zaidi kwa kumpachika jina la Ronaldo wa bongo 'Nado', wakimfananisha uchezaji wake na staa wa Juventus na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo.
Ni msimu wake wa kwanza akiwa na uzi maridadi wa Azam FC, alisajiliwa akitokea Mbeya City msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili, hadi sasa akionekana kuwa nguzo muhimu kwenye kiungo cha ushambuliaji kwenye kikosi cha timu hiyo.
Hadi sasa ligi ikiwa imesimama kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya CORONA, msimu huu kwenye mashindano yote Nado ametupia jumla ya mabao saba na kuchangia bao moja.
Nado amefunga mabao matano kwenye ligi na mawili kwenye Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup), akiiongoza Azam FC kutinga fainali ya tatu mfululizo ya michuano hiyo.
Kwa namna ulivyouona uwezo wake hadi sasa, nini kinakufurahisha kutoka kwake na kitu gani ungependa kumshauri akiongeze ili afikie mafanikio zaidi?

Post a Comment

0 Comments