BETI NASI UTAJIRIKE

MANARA AWAPIGA MKWARA MZITO WACHEZAJI SIMBA



Ofisa Habari wa Klabu ya Simba Haji Manara, amesema kuwa wachezaji wa Simba kwa sasa wakihojiwa na vyombo vya habari wanapaswa wazungumzie maisha yao binafsi na sio masuala ya Simba.

Akizungumza leo alipotembelea Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori Manara amesema huo ni utaratibu mpya ambao umewekwa baada ya kufanyika mabadiliko.

Manara amesema wachezaji wa timu ya Simba kwa sasa wakitaka kufanya mahojiano na vyombo vya habari hawapaswi kuigusa timu ya Simba.

"Mchezaji akiwa anafanyiwa mahojiano na vyombo vya habari anatakiwa kuongelea maisha yake binafsi na sio kugusa timu ya Simba vinginevyo anatakiwa kuomba ruhusa kutoka kwa uongozi wa timu hiyo," amesema.

Post a Comment

0 Comments