Alliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC Jackson Mayanja inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara amesema kuwa amewapa wachezaji wake mazoezi ya kucheza na wake zao wakiwa nyumbani ili kulinda vipaji vyao wakati huu ligi ikiwa imesimama.
Mayanja kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya KFC ya Uganda inayoshiriki Ligi Kuu ya Uganda amesema kuwa ameamua kuwapa wachezaji wake program maalumu watakazofanya nyumbani wakiwa na wake zao.
“Kwa sasa hakuna tena mkusanyiko wetu kwa ajili ya kuonana na wachezaji na kufanya nao mazoezi ila nimewapa program maalumu ambayo wataifanya nyumbani wakiwa na wake zao lengo ni kuona kwamba wanakuwa bora.
“Kwa kufanya hivyo itawasaidia kuyafurahia mazoezi wakiwa nyumbani na pale ligi itakaporejea tutarejea kwenye kasi yetu kwani ushindani nina amini utakuwa mkubwa ingawa haijajulikani ligi itarejea lini,” amesema.
Mayanja alikiongoza kikosi hicho kutoka kwenye nafasi ya 16 hadi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uganda pia amefanikiwa kukifikisha Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho nchini Uganda.
0 Comments