BETI NASI UTAJIRIKE

NGASSA AJICHIMBIA ZAKE MWANZA ,AELEZA ANACHOKIFANYA


Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa yuko jijini Mwanza akijifua lakini pia akichukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona.Mkongwe huyo mwenye historia ya pekee kunako klabu ya Yanga, amesema anaendelea na mazoezi binafsi ili kujiweka fit
Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona

"Kwa sasa niko Mwanza, pamoja na masuala mengine yaliyonileta, naendelea kufuata program ya mazoezi niliyoachiwa na Mwalimu. Ni vyema kila mmoja wetu akaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ili maisha yarudi kama zamani," amesema

Ngasa ni mmoja wa wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukingoni ndani ya kikosi cha Yanga.Bado mazungumzo ya mkataba mpya hayajaanza, lakini upo uwezekano mwamba huyo wa ziwa Victoria akaongezwa mwaka mmoja

Post a Comment

0 Comments