BETI NASI UTAJIRIKE

KASEKE AENDELEA KUPIGA KAZI NYUMBANI ,AZUNGUMZIA PROGRAMU YAKE




Bado haijafahamika ni lini Ligi itaweza kurejea kutokana na janga la virusi vya Corona kuendelea kuitesa dunia.Jana TFF ilitangaza kusogeza mbele muda wa kumalizika ligi kuu ya Vodacom kutoka Mei 30 hadi Juni 30

Wachezaji wa timu zote wako majumbani wakiendelea na mazoezi binafsi ili kujiweka fiti na tayari kurejea dimbani ligi itakapoanza.Kiungo mshambuliaji wa Yanga Deus Kaseke amesema yeye anatekeleza program aliyoachiwa na kocha Luc Eymael

Kaseka ambaye yuko mkoani Mbeya, amesema ratiba yake ya mazoezi huifanya asubuhi na jioni hupata muda wa kupumzika

"Kwa wachezaji wa Yanga kuna program ambayo kila mchezaji alipewa na kocha, kwa hiyo mimi ndio ninayoifata. Asubuhi nafanya mazoezi ya gym halafu napumzika vizuri kwa kulala, jioni napumzika"

"Kila mchezaji anajua wajibu wake kwa sababu kazi ya mpira ndio inampa kipato cha kuendesha maisha ya familia kwa hiyo naamini kila mchezaji anajitambua na ligi ikirudi kila mtu atakuwa kwenye hali nzuri," aliongeza Kaseke

Kuna wasiwasi kuwa mapumziko haya ya muda mrefu huenda yakaathiri mwenendo wa wachezaji ambapo kwa wale ambao hawatafanya mazoezi ipasavyo wanaweza kuongezeka uzito

Post a Comment

0 Comments