Uongozi wa klabu ya Simba unaandaa utaratibu wa kuwarejesha nchini wachezaji wake ambao wako nje ya nchiMtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema baadhi ya nyota wa kigeni wa timu hiyo walipewa ruhusa kurejea kwenye nchi zao kujiunga na timu za Taifa
Lakini kutokana na janga la Corona, baadhi ya nchi zimefunga mipaka yake na kuzuia safari kutoka kwenye nchi hizo hivyo kuwaweka nyota hao kwenye wakati mgumu
"Wachezaji wetu waliosafiri nje ya Tanzania, kabla ya mechi zetu mbili dhidi ya Azam na Yanga, tulipokea barua za wachezaji kuhitajika na timu zao za taifa kwa ajili ya kufuzu michuano ya AFCON. Tulipokea barua kutoka Kenya, Zambia, Rwanda, Msumbiji, Sudan na kama tungewazuia tungeadhibiwa na FIFA," amesema Senzo
"Wakati tunawaruhusu, serikali ya Tanzania ilikuwa bado haijatoa maamuzi juu ya janga la Corona kuwa wageni wakifika lazima waingie karantini kwa hiyo kwa sasa tunaangalia njia gani wataweza kurudi kwa wakati wakae karantini halafu wajiunge na timu"
Wachezaji ambao wako nje ya nchi ni Meddie Kagere (Rwanda), Francis Kahata (Kenya), Luis Miquissone (Msumbiji) na Sharaff Shiboub (Sudan)
0 Comments