advertise with us

ADVERTISE HERE

JANGA LA CORONA LINAVYOZIDI KUWAHARIBIA RAHA WATU WA SIMBAUongozi wa Simba umesema kuwa kikubwa ambacho wanakikosi kwa sasa ni zile furaha za mashabiki pamoja na uhondo wa mechi za Ligi Kuu Bara ambazo walikuwa wamezizoea.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kukosekana kwa uhondo huo kunawapa mawazo kidogo ila kwa kuwa ni kwa ajili ya afya hakuna namna lazima iwe hivyo.

"Unajua tayari kikosi cha Simba kilikuwa kwenye ubora wake na kwenye mechi zetu mbili za nyuma kabla ya ligi kusimamishwa tulishinda hivyo unaona hapo kulikuwa na ari na morali kiasi gani.

"Kwa sasa ambacho tunakikosa ni mechi pamoja na shangwe la wana Simba kushangilia ushindi wao, kikubwa na muhimu kwa sasa ni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ili kuwa salama kwani afya ni muhimu," amesema.

Wakati Ligi Kuu Bara inasimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Simba ilikuwa nafasi ya kwanza na pointi zake kibindoni 71.

Post a Comment

0 Comments