HUU NI WAKATI SAHIHI KWA BOCCO KUREJEA NYUMBANI AZAM?Uongozi wa Azam FC umesema kuwa ni wakati wa nahodha wa Simba, John Bocco kurejea Azam FC kwa kuwa ndio maskani yake ilipo.Bocco alijiunga na Simba msimu wa 2017 akitokea Azam FC yenye maskani yake Chamazi.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa ni wakati sahihi wa nyota huyo kurejea Azam kuendelea na soka.

"Bocco ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa akiwa uwanjani kwani anachokifanya kinaonekana, kwa sasa ni wakati wake kurejea Azam FC ili kurejea nyumbani," amesema.

 Msimu huu ndani ya Simba, Bocco amefunga mabao manne na kutoa pasi mbili za mabao.

Post a Comment

0 Comments