BETI NASI UTAJIRIKE

GSM WAAHIDI KUJA KIVINGINE NDANI YA YANGA


Wadhamini wa klabu ya Yanga SC kamuni ya GSM wamemaliza sintofahamu iliyokuwepo kati yao na uongozi wa Yanga . Mkurugenzi wa uwekezaji kampuni ya GSM amenukuliwa akisema .


Hatuna tofauti yoyote na Klabu ya Yanga SC, tumejitolea kuisaidia kama wanachama wao, kama yupo mwingine asaidie tunamkaribisha. Tutaendelea kuijenga Yanga nje na ndani, tutasajili mchezaji yoyote yoyote yule tukishirikiana na benchi la ufundi la Yanga"

"Kwa sasa tunasimamia mfumo wa mabadiliko ndani ya Yanga na tumewakodisha wataalamu kutoka Ulaya kuja kutusaidia kwa hili. Kuanzia mwezi Mei tutaanza ujenzi wa Uwanja kwa sasa Engineers wanashughulikia ramani ya uwanja"

"Tutahakikisha Yanga inakuwa na timu bora zaidi na kuleta ushindani ndani na nje ya Tanzania, tutaendelea kuijenga Yanga kimataifa. Hivi karibuni tutamleta mtaalamu mwingine wa mifumo ya Uwekezaji ili kuifanya Yanga iwe klabu kubwa na bora Afrika, Yanga imara nje na ndani"

"Kauli mbiu yetu sote iwe ni ubingwa msimu ujao, baada ya kuukosa kwa misimu mitatu mfululizo na njia pekee ya kuhakikisha tunatwaa ubingwa msimu ujao ni kuhakikisha tunasajili kikosi imara na kuhakikisha wachezaji wote walioonekana kuwa wanamchango kwenye klabu yetu msimu huu wanabaki"

Eng. Hersi Said

Post a Comment

0 Comments