EYMAEL AWATAJA WACHEZAJI 10 ANAOWATAKAKocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema ana majina ya wachezaji 10 ambao anawafanyia tathmini kuwajumuisha kwenye kikosi chake cha msimu ujao
Eymael amesema orodha hiyo inajumuisha wachezaji wa nje na wa ndani

Mbelgiji huyo ameshindwa kurejea nchini kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona, amesema lengo lake ni kutengeneza timu bora ambayo itafanya vizuri kwenye michuano yote watakayoshiriki msimu ujao

"Tunajaribu kuangalia na kufuatilia wachezaji wazuri wakati huu ili muda muafaka ukifika tusipate shida. Kwa maana hiyo nimekuwa na majina ya wachezaji wengi kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika ambao nimekuwa nikiwafatilia," amesema Eymael

"Siwezi kuyataja majina hayo wakati huu kwavile wengine bado wapo kwenye mikataba na timu zao, na pia tunaweza kuwataja wakati huu ikawa mbaya kwetu kwa timu nyingine zenye nguvu ya kifedha kwenda kuwapa ofa bora zaidi yetu na wakaenda huko.

"Pia hatuyataji kwa sababu inaweza kufika wakati ukapata mbadala bora zaidi ya yule uliyemtaja awali"

Pamoja na Mbelgiji huyo kugoma kutaja majina ya nyota anaowafuatilia, lakini inaelezwa tayari GSM imeanza kufanyia kazi mapendekezo yake kwa kuanza mazungumzo na baadhi ya wachezaji hao

Miongoni mwa nyota wa kigeni ambao inaelezwa Eyamael ametaka apatikane kwa gharama yoyote ni winga wa AS Vita Tuisila Kisinda

Kwa wachezaji wa ndani, miongoni mwa nyota aliowapendekeza ni pamoja na kiungo wa Azam Fc Salum Abubakar 'Sure Boy'
Lakini pia yupo mshambuliaji wa Namungo Fc Reliants Lusajo na viungo wa Mtibwa Sugar Salum Kihimbwa na Abdulkarim Humud

Hivi karibuni uongozi wa Yanga ulibainisha kuwa watasajili nyota wanne wa kigeni huku idadi ya wazawa ikitegemea na mahitaji ya timu baada ya mpango wa kuhuisha mikataba ya wachezaji ambayo inamalizika mwishoni mwa msimu

Post a Comment

0 Comments