Wakati hatma ya ligi kuu ikiendelea ikisubiri majaaliwa ya hali ya maambukizi ya Corona, wasiwasi umeanza kuibuka kuwa msimu unaweza usifike mwisho.Serikali ilisimamisha shughuli zote za michezo kwa muda wa siku 30 baada ya janga hilo kuingia nchini
Hata hivyo idadi ya maambukizi imeendelea kuongezeka huku Serikali ikiendelea kuchukua tahadhari kulinda usalama wa wananchi wake.Awali ligi ilitarajiwa kurejea mwezi huu lakini uamuzi huo utategemea na kauli ya Serikali pamoja na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF
Tayari TFF imetangaza kusogeza mbele tarahe ya kumalizika kwa ligi kutoka May 30 mpaka Juni 30.Kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF juzi, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo itafanya maamuzi ya mwisho kama ligi haitarejea ifikapo mwezi Juni
Changamoto ya Corona imeendelea kusitisha shughuli zote za michezo kwa karibu mataifa yote dunianiNchi ya Ubelgiji imekuwa ya kwanza kutangaza kumaliza msimu bila ya ligi kumalizika huku klabu ya Brugge iliyokuwa ikiongoza ligi kupewa ubingwa
Mamlaka za soka nchini humo zilitangaza uamuzi huo jana huku wakitangaza kuwa hakuna timu ambazo zitashuka daraja
0 Comments