Mshambuliaji wa Simba Miraji Athumani amesema amepona majeraha yaliyomuweka nje kwa zaidi ya miezi minne.Akihojiwa na mashabiki wa Simba kwenye kipindi cha ChatNa, Miraji alisema tayari ameanza mazoezi
"Namshukuru Mwenyez Mungu nimepona kabisa, najisikia kuwa na afya njema na tayari nimeshaanza mazoezi mepesi," alisema
"Nilikuwa na wakati mgumu kipindi chote nilichokuwa sichezi kwani nlitamani nami niingie uwanjani lakini ndio hivyo isingewezekana kutokana na majeraha"
"Ninaendelea kufanya mazoezi ili nikirejea kikosini niweze kuendeleza pale nilipoishia"
Katika mechi 10 alizoitumikia Simba mwanzoni mwa msimu kabla ya kupata majeraha, Miraji alifunga mabao sita na kusababisha mabao mengine manne
0 Comments