SENZO ATOA MAELEKEZO MAPYA KWA WACHEZAJI SIMBAUongozi wa klabu ya Simba umefikia uamuzi wa kuwaruhusu wachezaji waendelee kufanya mazoezi nyumbani mpaka pale TFF itakapotangaza tarehe ya kuanza ligi

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amebainisha kuwa wachezaji wamepewa program nyingine ya mazoezi ambayo wanapaswa kuifanya mpaka pale TFF itakapotangaza ligi kurejea

Senzo amesema kwa sasa ni muhimu kuweka kipaumbele kwa afya ya kila mmoja ili kuhakikisha wanakuwa salama na maambukizi ya virusi vya Corona

"Jambo muhimu zaidi kwa sasa ni kupambana na Corona ili isije ikaathiri kwenye timu yetu hasa kipindi cha kuanza mechi za ligi"

"Katika kikao chetu cha jana (juzi Jumanne) tuliwapa programu nyingine wachezaji wetu ili waendelee kuzifanya majumbani maana bado mapambano ya Corona ni makubwa hatuwezi kuwakusanya kipindi hiki"

"Programu hiyo ya kufanya mazoezi binafsi huko waliko itaendelea hadi hapo ambapo TFF litakapotangaza tarehe ya kuanza kwa ligi, hivyo hatuwezi kuingiza timu kwasasa bila kujua hilo," alisema Senzo

Post a Comment

0 Comments