Uongozi wa kiungo wa Simba Ibrahim Ajib, umeeleza kuwa hakuna ukweli wowote kuwa mteja wao ni mvivu wa mazoezi na hivyo kuwa sababu ya kutopewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha klabu ya Simba
Ajib aliyejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu akitokea klabu ya Yanga, ameshindwa kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Sven Vandenbroeck
Athumani Ajib, Wakala na kaka yake, amesema kuwa anaamini mteja wake ana uwezo mkubwa na pengine hapewi heshima yake kama anavyostahili
"Ajibu amekuwa akionesha uwezo mkubwa katika maisha ya soka licha ya kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimsema vibaya kuwa hajitumi akiwa kiwanjani"
"Watu wanadhani Ajibu hajitumi lakini sivyo, Ajibu anajali ratiba yake ya mazoezi na huwa anafika mazoezi mapema na hutekeleza kila anachoelekezwa na walimu wake"
"Muda utafika mashabiki wataiona thamani yake," alisema
Hivi karibuni kocha wa Simba Sven Vandenbroeck alieleza sababu ya kutompa nafasi ya Ajib kuwa hakuwa 'fit' kulinganisha na wenzake ambao wanacheza nafasi yake
Sven alimsifu Ajib kuna ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa lakini alimtaka aongeze bidii ili ampe nafasi mara kwa mara
Hata hivyo katika mechi ambazo Sven alimpa nafasi, Ajib alifanya vizuri
Changamoto ya kupata nafasi kwenye kikosi cha Simba pengine inatokana na ubora wa wachezaji wa timu hiyo hasa sehemu ya kiungo cha ushambuliaji ambayo Ajib hucheza
0 Comments