BETI NASI UTAJIRIKE

NYOTA WANNE KUTOLEWA KWA MKOPO SIMBA



Kocha Mkuu wa Simba Sven Van der broeck tayari amewasilisha mapendekezo yake ya usajili kuelekea msimu ujao Wakati huu Simba inaendelea na michakato ya kuhuisha mikataba ya wachezaji iliyomalizika lakini Sven amependekeza baadhi ya wachezaji ambao bado mikataba yao haijamalizika, watolewe kwa mkopo kwenda timu nyingine

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amefichua kuwa katika usajili watakaofanya watazingatia pendekezo hilo la Sven.Nyota kama Ibrahim Ajib, Kennedy Juma, Yusufu Mlipili, Said Ndemla na Rashid Juma ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa na nafasi finyu kwenye kikosi cha kwanza Simba

Ndemla na Mlipili mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu, mazungumzo ya kuwapa mikataba mipya inaelezwa yapo

Hata hivyo kwa Ndemla huenda kukawa na ugumu kwani nyota huyo anajiandaa kuelekea nchini Sweden.Lakini pia klabu ya Polisi Tanzania inatajwa kumtaka kiungo huyo mwenye msuli wa kupiga mashuti

Post a Comment

0 Comments