BETI NASI UTAJIRIKE

KAHATA ,CHAMA ,KAGERE NGOMA NGUMU KUREJEA NCHINI



Nyota wa kigeni walioruhusiwa kurejea makwao baada ya Serikali kusitisha shughuli za michezo kwa muda wa siku 30 kutokana na janga la Corona, wameshindwa kurejea kutokana na changamoto walizokutana nazo kwenye nchi zao

Nyota wa kigeni ambao walirejea makwao ni pamoja na Meddie Kagere (Rwanda), Francis Kahata (Kenya) na Clatous Chama (Zambia)

Rwanda ilisitisha safari zote kwa muda wa siku 30 ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo ambayo yanaenea kwa kasi kwenye nchi hiyo ndogo zaidi ukanda wa Afrika Mashariki
Hata Kenya na Zambia nako inaelezwa kuwa kuna masharti makali yamewekwa kwa wale wanaotaka kusafiri kwenda nje ya nchi hizo

Aidha, watakaporejea nchini wanapswa kukaa kwenye karantini kwa muda wa siku 14 kabla ya kuruhusiwa kuingia 'uraiani'

Uongozi wa klabu ya Simba jana ulitarajiwa kukutana kuandaa utaratibu mpya kwa wachezaji na watumishi wake ambao wote waliondolewa kazini kwa muda wa siku saba
Mkutano huo pia ulitarajiwa kuwahusisha wachezaji ambao walipaswa kuripoti kuanzia jana March 31

Post a Comment

0 Comments