BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAJIPANGA KUJENGA UWANJA WA KIHISTORIA AFRIKA MASHARIKI



Yanga imefanya tathmini ya viwanja vyote vikubwa jijini Dar es Salaam ukiwemo ule wa Azam Complex na wametamka wanakuja na bonge la sapraizi kwa mashabiki wao.

Vigogo wa Yanga wamesisitiza hawakwenda kwenye viwanja hivyo kujifurahisha bali kusoma mazingira na kuyajumuisha wakiwa na wataalam wa hali ya juu kuhakikisha wanakuja na kitu cha tofauti kabisa pale Kigamboni.

Ujenzi wa mradi huo umepewa jina la ‘ Kigamboni Sports Complex home of Champions’ unaanza mwezi Juni mwaka huu na hasa baada ya kipindi cha mvua kumalizika ili kuepusha usumbufu.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Ujenzi na Miundombinu wa Yanga, Said Mrisho alisema;

"Tunataka Yanga iwe klabu ya mfano ambao unaendana na hadhi ya jina lake. Ni klabu ambayo ina historia kubwa sana nchini, kwa hiyo hata wageni wakija kuitembelea, wawe wamekutana na kitu cha kihistoria na kwenda kusimulia huko waendako."

Alifafanua uongozi wa Yanga umejipanga kuhakikisha mradi huo unaanza na kuwa na kasi kubwa ili kukamilika kwake.

Mrisho pia alisema suala la bajeti na wapi klabu itapata fedha halina tatizo. Awali walikuwa na mpango wa ujenzi wa uwanja wa mazoezi eneo la Jangwani (Kaunda), lakini waliamua kusitisha zoezi hilo kutokana na mradi mkubwa wa serikali ambao utafanyika katika eneo hilo.

Mrisho alisema wanaamini kuwepo kwa mradi huo, klabu itafaidika nao kwani tatizo kubwa la mafuriko litakuwa limepatiwa ufumbuzi na wao kuanza mpango wa kujenga uwanja wa mazoezi eneo hilo ambao utatumika zaidi na timu ya vijana na ya wanawake.

Alisema kuwa mchoro wa uwanja wa Kigamboni umekamilika na utakuwa na viwanja viwili kimoja cha nyasi bandia na kingine cha nyasi za asili.

Alisema kuwa viwanja vyote hivyo havitafanana na vya klabu nyingine ukiwemo ule wa Azam Complex ambao unaonekana wa kisasa na gharama zaidi nchini. Kwa mujibu wa Mrisho kiwanja cha mazoezi kitakuwa na vifaa vya kisasa ikiwa pamoja na gym na Sauna.
Sambamba na hayo, pia kutakuwa na uwanja wa mpira wa kikapu, mpira wa wavu na bwawa la kuogelea la mita 50 linalokidhi viwango vya Kamati ya Olimpiki Duniani (IOC), Michezo ya Madola na Shirikisho la kuogelea duniani (Fina).

Alisema lengo la kujenga bwawa la kuogelea ni kuwawezesha waogeleaji wa Tanzania kuweka kambi

Post a Comment

0 Comments