BETI NASI UTAJIRIKE

NIYONZIMA ATOA MAAGIZO KWA WACHEZAJI WOTE YANGA



Wakati huu ligi ikiwa imesimama katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, nyota wa Yanga walipewa ruhusa ya kurejea makwao ambapo pamoja nayo, walipewa program maalum za mazoezi kwa kila mmoja

Kiungo mnyumbufu Haruna Niyonzima amesema yeye amekuwa akizingatia program hiyo na amewasisitizia wachezaji wengine kuhakikisha wanaifuata ili watakaporejea wawe timamu kwa ajili ya mapambano

Niyonzima amesema mechi zilizosalia kumaliza msimu zote zitakuwa ngumu kutokana na ushindani uliopo hasa kukiwa na timu nyingi ambazo zinajinusuru kuteremka daraja
Lakini pia Yanga inabaliwa na michezo ya kombe la FA, michuano ambayo wanahitaji kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao

"Nashauri wachezaji wenzangu kujituma na kufanya mazoezi ili kuiweka miili sawa katika kipindi hiki cha mapumziko, tunahitaji kurejea na nguvu na si kuanza upya", 
alisema Niyonzima.

Mnyarwanda huyo alisema endapo mchezaji yoyote atakaa bila ya kufanya mazoezi, atajiweka kwenye wakati mgumu mara mechi za Ligi Kuu Bara zitakaporejea tena.

"Nafahamu athari za kutokufanya mazoezi, nikikaa bila mazoezi mwili utakuwa mzito na mwisho wa siku nitashindwa kuitumikia timu yangu katika kiwango kizuri"

Ligi inatarajiwa kuendelea baada ya April 17 lakini itategemea na hali ya maambukizi ya virusi vya Corona pamoja na maelekezo ya Serikali

Post a Comment

0 Comments