WACHEZAJI WATATU AZAM FC WALAMBA MIKATABA YA UHAKIKA
Azam FC imewapa mikataba mipya wachezaji wake chipukizi watatu, mabeki Oscar Maasai, Lusajo Mwaikenda na mshambuliaji Andrew Simchimba.
Watatu hao zao la akademi ya timu, walisaini mkataba wa miaka mitatu kila mmoja jana chini ya Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, ofisi kuu ya klabu hiyo, barabara ya Nyerere, Dar es Salaam.
Lusajo alikuwa akimaliza mkataba wake wa awali Septemba mwaka huu, na sasa mkataba huo mpya utamfanya aendelee kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ (kulia) akisaini mkataba na Andrew Simchimba jana Jijini Dar es Salaam 

Beki huyo amekuwa na mwendelezo mzuri wa kipaji chake tokea ajiunge na Azam Academy hadi kupandishwa timu kubwa msimu uliopita.
Masai aliyekulia kwenye akademi ya Azam, amekuwa msaada katika nafasi ya beki wa kati kila mara anapopewa nafasi tokea apandishwe timu kubwa msimu uliopita.
Awali mkataba wa Simchimba ulikuwa unamalizika Septemba mwaka huu, ambapo baada ya kurefushwa unatarajia kumalizika 2023.
Na Simchimba amekuwa na kiwango kizuri tokea ajiunge na Azam Academy kabla ya msimu uliopita kutolewa kwa mkopo Coastal Union alipoendelea kufanya vema.
Baada ya benchi la ufundi la Azam FC kuridhishwa na uwezo wake, waliamua arejee kwenye kikosi cha wakubwa cha timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo Desemba mwaka jana.Beki Lusajo Mwakenda amesaini mkataba mpya wa miaka miatu kuendelea kufanya kazi Azam FC Beki Oscar Maasai amesaini mkataba mpya wa miaka miatu kuendelea kufanya kazi Azam FC 

Post a Comment

0 Comments