DKT.MSOLLA APEWA TANO NA WENYE YANGA YAOViongozi wa Matawi ya klabu ya Yanga wamempongeza Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla kwa kuchukua hatua ya kuwaondoa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliosababisha mtafaruko ambao ulipelekea Wadhamini wa klabu hiyo kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa

Mratibu wa Matawi, Kais Edwin amesema wao walitoa ombi na wanashukuru uongozi umelifanyia kazi haraka iwezekanavyo kwa manufaa ya Klabu ya Yanga.
Amesema Dk Msolla kaonyesha ukomavu katika uongozi kwa kuwachukulia hatua wahusika hao

"Tulisema kwa kumaanisha, ila Dk Msolla kiongozi msikivu, kalifanyia kazi sasa tunamuomba GSM arejeshe moyo wake nyuma na kuendelea kuisapoti Yanga, haya yamepita arejee kama alivyokuwa akifanya"

Juzi na jana Kamati ya Utendaji ya Yanga ilijifungia nje ya ofisi za Klabu hiyo siku mbili mfululizo kujadili sakata hilo na ndipo jana jioni ikatoka na maazimio ya kuwasimamisha wajumbe wawili huku watatu wakitangaza kujiuzulu wenyewe.

Post a Comment

1 Comments