BODI YA LIGI YAJA NA MBINU MPYA MECHI YA YANGA VS SIMBAUtaratibu mzuri umewekwa ili kuwafanya mashabiki waingie uwanjani kwa amani na utulivu
JINSI MAMBO YALIVYOPANGWA
1. Nunua tiketi yako mahali popote Tanzania kupitia Mawakala wa Selcom.

2. Milango itakuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi na watu wataruhusiwa kuingia uwanjani.

3. Barabara itakayotumika kwa wale wenye Magari ni Mandera Road. Barabara ya kutokea Chang'ombe DUSE itafungwa kwa matumizi ya  magari bali watu wataruhusiwa kuingia kwa miguu.

4. Magari yatakayoingia Uwanjani ni yale ambayo yatakuwa na Sticker maalumu tu ambayo Jumla yake ni 150.

5. Maeneo yaliyotengwa kwa maegesho ya magari ni Chuo cha Uhasibu, Viwanja vya Sabasaba, Chang'ombe na maeneo mengine ya Jirani. Mpenzi mshabiki hakikisha unaegesha gari lako mahali salama.

6. Wakati wa kuingia hakikisha unakaa kwenye Mstari ukiwa na tiketi yako mkononi.
Watu watakaoscan tiketi yako ni SUMA JKT ambae ana Uniform, epuka kuscaniwa Tiketi na Mtu yoyote ambaye sio SUMA JKT

Polisi kazi yao ni Usalama wa mali na watu na hawatakuwa wakiscan tiketi ZINGATIA.

BEI RASMI YA TIKETI NI
VIP A 30,000
VIP B NA C 20,000
ORANGE 10,000
GREEN 7,000

Post a Comment

0 Comments