Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kusikitishwa na kauli iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda akiituhumu klabu ya Yanga kuwa ilitumia dawa kwenye mchezo dhidi ya Simba
Katika mchezo huo uliopigwa March 08 kwenye uwanja wa Taifa, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.juzi wakati akiikabidhi KMC kitita cha Tsh Milioni 20 baada ya kuifunga Yanga, Makonda alieleza kushangazwa na nguvu walizokuwa nazo Yanga kwenye mchezo dhidi ya Simba
"Hii mechi ya Simba na Yanga tulifungwaje mpaka keshokutwa sielewi. Najiuliza hawa watu hii nguvu waliitoa wapi? Mpaka leo natamani ya kwamba tuanze kuweka kakipimo pale uwanja wa Taifa ili kila mtu anatema mate kabla ya kucheza," alisema Makonda
Kauli hiyo imelaaniwa vikali na wadau wa soka nchini kwani kwa nafasi yake, pamoja ya kuwa ni mshabiki na mshauri wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, hapaswi kutumia nafasi yake kwa namna yoyote kuikandamiza timu nyingine ya mkoa wake
Mh Makonda anapaswa kuwa mlezi wa timu zote za mkoa wa Dar es salaam
0 Comments